Endapo tutasema Professor Jay amerudi tena au hata tuiweke kwa kimombo kwamba Professor Jayis back ili kuonyesha msisitizo,bila shaka tutakuwa tunakosea.Nasema hivyo kwa imani moja nyepesi kabisa; Professor Jay alikuwepo,yupo na hakuna ubishi kwamba ataendelea kuwepo.
Hii ni kutokana na jinsi ambavyo kwa muda mrefu Professor Jay(jina kamili Joseph Leonard Haule) amekuwa akifanya kama kupotea hivi kabla hajaibuka upya kama sio kivingine kabisa kama ambavyo amefanya katika wimbo ambao nina furaha kuutambulisha kwako hivi leo.
Wimbo unaitwa Kamili Gado,ambalo ni neno la kimtaa kidogo lenye kumaanisha kitu au mtu aliyeko kamili katika mengi. Huu ni wimbo wa pili rasmi kutoka katika album yake mpya inayokwenda kwa jina Jayscoambayo kwa mujibu wake,maandalizi kabambe ya kuiweka uwanjani yanaendelea.
Katika wimbo huu ambao umetengenezwa pale MJ Records(Masaki jijini Dar-es-salaam),Professor Jay amemshirikisha Producer wa wimbo huo,Marco Chali. Usikilize wimbo KamiliGado kwa kubonyeza player hapo chini na kisha tembelea tovuti maalumu ya wimbo huu,www.kamiligado.com kwa ajili ya kudownload wimbo wenyewe,Instrumental na Acapella.Kumbuka tu kwamba hiyo yote ni kwa ajili ya Promotions tu na sio matumizi mengineyo.

No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.