“Mradi huu utamaanisha usambazaji bora na wa kuaminika, unaopunguza makosa na usumbufu katika mfumo wa usambazaji,” alisema Joseph Njoroge, ambaye ni meneja mkurugenzi wa Shirika la Umeme la Kenya.
Laini za umeme za juu ya ardhi sasa zitahamishiwa chini ya ardhi, kwa kuanzia na wilaya za biashara katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu. Hatua hiyo itapunguza kukatika kwa umeme kutokana na sababu za kimazingira na hali mbaya ya hewa, alisema Njoroge.
Nyaya za chini ya ardhi zinachukuliwa kuwa ni salama kwa mazingira kwa sababu zinaepusha matumizi ya nguzo na ukataji wa miti kwa ajili ya kusafisha njia ya laini ya umeme, na pia zinapunguza utoaji wa maeneo ya umeme, limeripoti gazeti hilo.

No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.