Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa
darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na
Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano
hilo.
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa kwenye
mafunzo ya vitendo yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving
School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo
Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji Kanda ya
kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei 5 2012 ndani
ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la
Arusha.
Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi
Upendo Simwita kutoka kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji
wa shindano hilo,amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na
kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka
sasa wametimia 20.
Bi Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato
wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo
hao wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss
Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.
“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya
nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani,
na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema Upendo.Amesema
kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh
25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya booking yako ya tiketi
mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.
Kwa upande wa Burudani,Upendo amesema kuwa kutakuwepo na
Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa
Asili,Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine mbalimbali
zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.
Upendo amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni
REDD’S ORIGINAL,NAURA SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB –
ARUSHA,BG HORIZON, MODERN
DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE & BEKI FOR LIFE, MWANDAGO
INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO SECURITY,GOLDEN ROSE HOTEL,RIVERSIDE
SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL LODGE,LITTLE ROSES, LA
BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.